Wednesday, February 10, 2016

ZAMALEK YAMTIMUA MIDO.

KLABU ya Zamalek ya Misri imemtimua kocha wake Ahmed Hossam maarufu kama Mido baada ya kupoteza mchezo wao dhidi ya mahasimu wao wa jiji la Cairo Al Ahly. Zamalek ambao walitandikwa mabao 2-0 katika mchezo huo uliochezwa jana, pia imemtimua mkurugenzi wa michezo Hazem Emam na kumteua Mohamed Salah kluwa kocha wa muda. Mido ambaye pia amewahi kucheza katika klabu ya Tottenham Hotspurs, aliwahi kuwa mshambuliaji wa Zamalek kabla ya kustaafu soka mwaka 2013. Aliteuliwa kuwa kocha wa klabu hiyo Januari mwaka 2014.

No comments:

Post a Comment