Wednesday, February 10, 2016

WAKALA WA TURAN AKANUSHA TETESI ZA MTEJA WAKE KUTAKA KWENDA CHINA.

WAKALA wa kiungo wa Barcelona, Arda Turan amekanusha taarifa kuwa mteja wake amepata ofa kutoka China. Taarifa za vyombo vya habari zimedai kuwa klabu ya Beijing Guoan inayoshiriki Ligi Kuu ya China ilikuwa ikijiandaa kutoa ofa ya kumlipa Turan kitita cha euro milioni 20 kwa msimu katika mkataba wa miaka mitano. Nyota huyo wa kimataifa wa Uturuki ndio kwanza ameanza kuitumikia Barcelona Januari toka asajiliwe akitokea Atletico Madrid kwa kitita cha euro milioni 34. Lakini wakala wake Ahmet Bulut amesisitiza kuwa hakuna ofa yeyote kutoka China waliyopata na mteja wake hana mpango wowote wa kuondoka Camp Nou kwasasa. Klabu za China zimekuwa zikitumia kiasi kikubwa cha fedha katika wiki za karibuni kwa kuwanasa Jakcson Martinez, Ramires, Luiz Adriano na Alex Teixeira ambao wote wametokea barani Ulaya kwenda Asia.

No comments:

Post a Comment