Wednesday, February 10, 2016

MOURINHO ADAIWA KUWAAMBIA MARAFIKI ZAKE KUWA ATAKWENDA MAN UNITED.

MARAFIKI na watu wa karibu wa Jose Mourinho wamedai kuwa kocha huyo amewahabalisha kuwa yeye ndio atakayechukua nafasi ya Louis van Gaal katika klabu ya Manchester United. Magazeti ya Uingereza yakiwemo Daily Mail, Daily Star, Daily Mirror na daily Telegraph yote yamewanukuu watu wasiojulikana wanaodaiwa kuwa karibu na Mreno huyo mwenye umri wa miaka 53, wakidai tayari ameshafikia makubaliano na United. Mourinho ambaye amewahi kuzinoa klabu za Real Madrid, Inter Milan na Porto alitimuliwa na Chelsea Desemba mwaka jana lakini katika mahojiano yake ya hivi karibuni amesema atarejea tena kufundisha hivi karibuni. Van Gaal ambaye atakuwa amebakisha mwaka mmoja kabla ya mkataba wake kumalizika ifikapo mwishoni mwa msimu huu, amekuwa akiandamwa na tetesi kuhusu mustakabali wake kutokana na matokeo mabovu ambayo United imekuwa ikipata.

No comments:

Post a Comment