Wednesday, February 10, 2016

MASHABIKI WA DORTMUND WARUSHA VITENESI UWANJANI KUPINGA BEI KUBWA YA TIKETI.

MASHABIKI wa Borussia Dortmund jana wametupa mipira ya tenisi uwanjani wakati wa mchezo wa Kombe la DFB dhidi ya Stuttgart kupinga bei kubwa ya tiketi. Mashabiki hao pia waligoma kuingia uwanjani dakika 20 za kwanza za mchezo huo ambapo Dortmund walishinda mabao 3-1. Mashabiki hao wamedai kutofurahishwa na gharama kubwa za tiketi katika michezo ya Bundesliga. Jumamosi iliyopita mashabiki wa Liverpool nao walitoka nje ya uwanja wa Anfield katika mchezo dhidi ya Sunderland kupinga suala hilohilo la gharama kubwa za tiketi.

No comments:

Post a Comment