Tuesday, February 9, 2016

LIGI KUU UINGEREZA KUTUMIA NEMBO MPYA MSIMU UJAO.

LIGI Kuu ya Uingereza imebainisha muonekano wake mpya ambao utatumika kuanzia msimu wa 2016-2017. Picha ya Simba ndio iliyokuwa ikionekana kama nembo ya ligi hiyo toka ilipozinduliwa mwaka 1992 lakini sasa inatarajiwa kufanyiwa mabadiliko ili kuweka muonekano wa kisasa zaidi. Klabu zote 20 zinazoshiriki ligi hiyo pia zimekubali mikakati mipya ya udhamini ambayo inamaanisha kuwa ligi hiyo haitakuwa tena na jina la mdhamini. Kampuni ya Barclays waliokuwa wadhamini wakuu wa ligi hiyo wameamua kutoongeza mkataba wa udhamini pindi ule wa sasa utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu.

No comments:

Post a Comment