Wednesday, February 10, 2016

ALLEGRI AKANUSHA TETESI ZA KWENDA CHELSEA.

MENEJA wa klabu ya Juventus, Massimiliano Allegri amekanusha taarifa zilizozagaa zikidai kuwa ndiye anayetarajiwa kuchukua nafasi ya meneja wa muda wa Chelsea Guus Hiddink mwishoni mwa msimu huu. Allegri ambaye aliiongoza Juventus kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita, ana mkataba unaomalizika Juni mwaka 2017 lakini anatajwa kuongoza katika orodha ya makocha wanaowindwa na Chelsea kuziba nafasi ya Jose Mourinho.  Taarifa nchini Uingereza leo zimedai mmiliki wa Chelsea Roman Abramovic ameondoa uwezekano wa kumchukua Diego Simeone kwasababu hapendezewi na aina ya mchezo anayotumia kocha huyo wa Atletico Madrid. Ingawa kocha wa zamani wa Juventus Antonio Conte naye pia amekuwa akihusishwa katika kinyang’anyiro hicho, lakini nyota imeonekana kumuwakia Allegri kutokana na mafanikio makubwa aliyopata mwaka jana.  Lakini mwenyewe alipohojiwa kuhusiana na suala hilo alikanusha akidai hakuna ukweli wowote katika hilo.

No comments:

Post a Comment