Friday, November 27, 2015

RODRIGUEZ KUKAA NJE MIEZI MIWLI.

MENEJA wa klabu ya Southampton, Ronald Koeman amethibitisha kuwa mshambuliaji Jay Rodriguez anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa miezi miwili baada ya kufanyiwa upasuaji wa mguu. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 alirejea katika kikosi hicho mwanzoni mwa msimu baada ya kukaa nje kwa zaidi ya mwaka mmoja akiuguzu majeruhi ya goti. Rodriguez amecheza mechi 12 msimu huu lakini hajacheza toka walipopata sare ya mabao 2-2 dhidi ya Leicester City Octoba 17 mwaka huu. Wakati huohuo Koeman amekanusha tetesi zilizozagaa kuwa watamuuza mshambuliaji wao Sadio Mane akihusishwa kuhamia Chelsea au Manchester United. Koeman amesema hawana mpango wa kuuza mchezaji yeyote katika kipindi cha dirisha dogo la usajili Januari mwakani.

No comments:

Post a Comment