Friday, November 27, 2015

RAIS WA CBF AJIUZULU WADHIFA WAKE FIFA.

RAIS wa Shirikisho la Soka la Brazil-CBF, Marco Polo Del Nero amejiuzulu wadhifa wake kama mjumbe wa kamati wa utendaji ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA anayewakilisha Shirikisho la Soka la Nchi za Amerika Kusini-Conmebol. Katika taarifa yake Conmebol ilithibitisha taarifa hizo ikidai kuwa sababu haswa ni shinikizo alilokuwa nalo kwa miezi kadhaa na nafasi yake itachukuliwa na Fernando Sarney. Sarney ni mtoto wa rais wa zamani wa Brazil na mmoja kati ya makamu wanne wa rais wa CBF. Del Nero alichukua mikoba ya Jose Maria Marin kuiongoza CBF Aprili mwaka huu na ataendelea na wadhifa wake huo.

No comments:

Post a Comment