Friday, November 27, 2015

CABALLERO ATAMBA KUZIBA PENGO LA HART.

GOLIKIPA wa akiba wa Manchester City Willy Caballero ana uhakika anaweza kuziba nafasi ya Joe Hart kama ya majeruhi ya kipa huyo namba moja wa Uingereza aliyopata katika mchezo dhidi ya Juventus Jumatano yatamuweka nje katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Southampton. Hart alipata majeruhi ya msuli wa paja katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na kutolewa nje kumpisha Caballero katika dakika ya 81 na kuna uwezekano pia wa kuukosa mchezo wa kesho. Akihojiwa Caballero amesema hajapenda Hart aumie lakini anapaswa kujiandaa kwasababu hayo ndio maisha ya kipa wa akiba. Caballero aliendelea kudai kuwa ni vizuri kucheza michezo kadhaa mfululizo lakini hilo litategemea na jinsi hali ya Hart itakavyokuwa.

No comments:

Post a Comment