Friday, November 27, 2015

ANELKA 'MZEE WA KUHAMAHAMA' ANATAFUTA KLABU NYINGINE.

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Anelka yuko mbioni kutafuta klabu nyingine baada ya kushindwa kuiongoza Mumbai City kutinga hatua ya mtoano ya Ligi Kuu ya India. Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 36 amekuwa kocha-mchezaji wa Mumbai ambao waling’olewa katika msimu wa pili wa ligi hiyo yenye timu nane baada ya sare ya bao 1-1 waliyopata nyumbani dhidi ya Kerala Blasters jana. Akihojiwa baada ya sare hiyo Anelka ambaye kuzichezea Arsenal, Real Madrid na Chelsea amesema hadhani kama ataendelea tena na kibarua chake. Anelka aliongeza kuwa lengo lao ilikuwa ni kufika hatua ya nusu fainali na lengo hilo halijafikiwa hivyo hajui kitu gani kitatokea dhidi yake.

No comments:

Post a Comment