Friday, October 9, 2015

VIGOGO BRAZIL NA ARGENTINA ZAANGUKIA PUA MECHI ZA KUFUZU.

VIGOGO wa soka Amerika Kusini, timu za Brazil na Argentina jana zimejikuta zikiangukia pua baada ya kutandikwa katika mechi zao za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018. Brazil ambao walikuwa bila nyota wake Neymar anayesakata kabumbu katika klabu ya Barcelona, walitandikwa mabao 2-0 ugenini na mabingwa wa Copa America Chile. Mambo yalikwenda hivyohivyo kwa Argentina mbao nao walikubali kipigo cha mabao 2-0 nyumbani kutoka kwa Ecuador ambao nao walikuwa wakicheza bila nyota wake wa Barcelona Lionel Messi aliyekuwa majeruhi. Chile wao walipata ushindi wao kwa mabao yaliyofungwa na Eduardo Vargas na Alexis Sanchez mchezo ambao ulifanyika huko Santiago. Jijini Buenos Aires, wageni Ecuador waliondoka na ushindi huo kwa mabao yaliyofungwa na Frickson Erazo na Felipe Caicedo.

No comments:

Post a Comment