Friday, October 9, 2015

MESSI KUSIMAMA KIZIMBANI KAMA KAWAIDA.

MAHAKAMA nchini imeamuru mshambuliaji nyota wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi na baba yake kusimama kizimbani na kujibu mashitaka ya ukwepaji kodi. Jaji anayesimamia kesi hiyo alikataa ombi la waendesha mashitaka kumuondolea mashitaka mshambuliaji huyo. Messi na baba yake Jorge wanatuhumiwa kwa kukwepa kodi zaidi ya euro milioni nne, tuhuma ambazo hata hivyo wamezikataa. Wakili wa upande mshitaka ametaka watuhumiwa wote wawili kupewa vifungo vya miezi 22 jela kama wakikutwa na hatia ya kutenda kosa hilo. Waendesha mashitaka wanamtuhumu Jorge kukwepa kodi ya mapato ya mwanae aliyopata kwa kutumia kampuni za nje huko Belize na Uruguay kati ya 2007-2009. Mawakili wa Messi wamesema mchezaji huyo hajawahi kutumia hata dakika moja katika maisha yake kusoma, kujadili au kuchambua mikataba.

No comments:

Post a Comment