Friday, October 9, 2015

KUFA NA KUPONA MAREKANI NA MEXICO KESHO.

TIMU za taifa za Marekani na Mexico zinatarajiwa kukwaana huko Pasadena kesho ambapo mshindi katika mchezo huo atakuwa amepata nafasi ya moja kwa moja kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho nchini Urusi mwaka 2017. Zaidi ya tiketi 92,000 tayari zimeshauzwa kwa ajili ya mchezo huo unaowakutanisha miamba ya Amerika Kaskazini utakaofanyika katika Uwanja wa Rose Bowl. Mchezo huo ni mahsusi kwa ajili ya kutafuta mwakilishi kutoka nchi za Shirikisho la Soka la Amerika Kaskazini, Kati na Caribbean-Concacaf, baada ya Marekani kushinda Kombe la Gold mwaka 2013 huku wenzao Mexico wao wakishinda taji hilo mwaka huu. Marekani ilishindwa kutetea taji hili mwaka huu katika ardhi yao baada ya kuondoshwa na Jamaica katika hatua ya nusu fainali. Tayari kocha wa Marekani Jurgen Klinsmann ameanza kukosolewa kutokana na kiwango duni kilichoonyeshwa na timu hiyo katika mechi zake hivi karibuni, huku wadau wengi wakidai anapaswa kutimuliwa kama akishindwa katika mchezo huo wa kesho.

No comments:

Post a Comment