Friday, October 9, 2015

KLOPP AWAONDOA HOFU WACHEZAJI WA LIVERPOOL.

MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp amesisitiza anafurahia kikosi alichonacho hivi sasa na hana mpango wa kuangalia usajili wa ndoto wa kina Lionel Messi au Cristiano Ronaldo. Klopp amechukua mikoba ya Brendan Rodgers wakati Liverpool ikijaribu kujipanga upya kufuatia kuanza msimu kwa kusuasua na kupelekea kushinda mechi tatu pekee kati ya nane za Ligi Kuu msimu huu. Akihojiwa Klopp amesema ndio kwanza anaanza hivyo hana mpango wowote wa kuwaza kusajili kwasababu ana uhakika kikosi alichokabidhiwa ni kizuri. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa anataka kuanza kazi na wachezaji waliopo hivyo atawaomba ushirikiano wao ili waweze kurejea katika kiwango chao. Klopp mwenye umri wa miaka 48 ambaye ametia saini ya mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya paundi milioni 15 amesema anafahamu changamoto iliyopo mbele yake haswa ikizingatiwa Liverpool ni klabu kubwa katika ulimwengu wa soka.

No comments:

Post a Comment