Friday, October 9, 2015

BLATTER AKATA RUFANI KUPINGA KUSIMAMISHWA SIKU 90.

GAZETI la New York Times limeripoti kuwa Sepp Blatter amekata rufani rasmi dhidi kusimamishwa kwake na Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. Blatter ambaye amekuwa rais wa FIFA toka mwaka 1998 alisimamishwa jana na kamati hiyo kwa siku tisini kufuatia uchunguzi wa kihalifu unaendelea dhidi yake. Taarifa ya gazeti hilo la Marekani imedai kuwa Blatter amekata rufani hiyo akidai kutotendewa haki kwani kamati haikumuita na kumuhoji kuhusiana na tuhuma zinazomkabili. Mawakili wa Blatter nchini Uswisi na Marekani hawakupatikana mara moja ili kutoa kauli zao kuhusiana na taarifa hizo. Mwanasheria Mkuu wa Uswisi amesema Septemba 25 mwaka huu walifungua ya kihalifu inayomhusu Blatter wakimtuhumu kuidhinisha kiasi cha euro milioni mbili kutoka FIFA kumuendea rais wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA Michel Platini pamoja na haki za matangazo za Caribbean.

No comments:

Post a Comment