Friday, October 9, 2015

AGUERO PANCHA TENA.

MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Sergio Aguero amepata majeruhi ya msuli wa paja wakati akiitumikia timu yake ya taifa ya Argentina ambayo ilichapwa mabao 2-0 katika mechi ya kufuzu michuano ya Kombe la Dunia 2018 dhidi ya Ecuador jana. Aguero ambaye alifunga mabao matano katika ushindi wa City dhidi ya Newcastle Octoba 3 mwaka huu, alitolewa nje na machela katika dakika ya 22 ya mchezo huo. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 anatarajiwa kufanyiwa vipimo ili kujua ukubwa wa tatizo na anatarajiwa kukosa mchezo mwingine wa nchi yake dhidi ya Paraguay wiki ijayo. City ambao ndio vinara wa Ligi Kuu kwasasa wanatarajiwa kukwaana na Bournemouth Octoba 17.

No comments:

Post a Comment