Sunday, July 5, 2015

PALACE YATHIBITISHA KUMUWINDA CABAYE.

MWENYEKITI msaidizi wa Crystal Palace, Steve Parish amethibitisha kuwa klabu hiyo inataka kumsajili Yohane Cabaye kutoka klabu ya Paris Saint-Germain-PSG. Inaaminika meneja wa Palace Alan Pardew anataka kuungana tena na kiungo huyo wa zamani wa Newcastle United aliyekuwa akimfundisha wakati akiwa St James Park. Tayari kuna taarifa kuwa Roma nao tayari wameulizia uwezekano w kumsajili nyota huyo majira haya ya kiangazi lakini Parish anaamini watashinda katika mbio hizo. Parish amesema mipango yao ni kuhakikisha wanapata nafasi 10 za juu katika msimamo wa Ligi Kuu msimu ujao hivyo ni lazima walete wachezaji bora watakaoweza kufanikisha hilo.

No comments:

Post a Comment