Sunday, July 5, 2015

GERRARD ATAMBULISHWA RASMI GALAXY.

NAHODHA wa zamani wa kimataifa wa Uingereza, steven Gerrard amekutana na mashabiki wake wapya wakati alipotambulishwa katika klabu ya Los Angeles Galaxy kwa mara ya kwanza jana akitokea Liverpool kwa uhamisho huru. Gerrard ambaye pia alikuwa nahodha wa Liverpool aliibuka uwanjani na kuwatakia mashabiki wa Galaxy heri katika sherehe za Julai 4 ambazo husheherekewa nchini kote Marekani huku timu yake ikifanikiwa kuichapa Toronto kwa mabao 4-0. Akizungumza alipopewa kipaza sauti wakati wa mapumziko Gerrard aliwaambia mashabiki hao kuwa anajisikia furaha kuwa nao na ana hamu kubwa ya kuvaa jezi ya timu hiyo na kuanza kuwatumikia. Gerrard atakutana tena na mchezaji mwenzake wa zamani wa Liverpool Robbie Keane ambaye aliibuka nyota ya mchezo kwa kufunga mabao matatu-hat-trick jana.

No comments:

Post a Comment