Tuesday, April 21, 2015

VILLA YASHITAKIWA NA FA KWA VURUGU.

KLABU ya Aston Villa imeshitakiwa na Chama cha Soka cha Uingereza-FA kwa mashabiki kuvamia uwanja mwishoni mwa mchezo wa robo fainali ya michuano ya Kombe la FA ambao walishinda mabao 2-0 dhidi ya West Bromwich. Baadhi ya mashabiki wa wa nyumbani walivamia uwanja wa Villa Park katika dakika za majeruhi na wakati mchezo umemalizika wakati viti vilipokuwa vikirushwa kutoka jukwaa la mashabiki wa West Brom Machi 7 mwaka huu. Katika tukio hilo wachezaji kadhaa wa West Brom walionekana kusukumwa na mashabiki waliokuwa wamevamia uwanjani. Klabu ya Reading nayo imeshitakiwa kwa kosa kama hilo baada ya mashabiki wake nao kuvamia uwanjani baada ya mchezo dhidi ya Bradford. Timu zote mbili zimepewa mpaka Aprili 23 mwaka huu kujibu tuhuma hizo kabla ya kulimwa adhabu.

No comments:

Post a Comment