Sunday, February 1, 2015

TETESI ZA USAJILI ULAYA: SPURS KUMFUKUZIA RODRIGUEZ, PALACE NA HULL ZAMMEZEA MATE LAMBERT, REUS ADAI ANAPENDA KUFANYA KAZI NA WENGER.

KATIKA habari za tetesi za usajili meneja wa klabu ya Tottenham Hotspurs Mauricio Pochettinho ana kitita cha paundi milioni 60 cha kutumia katika usajili na amepanga kuweka ofa kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji wa Southampton Jay Rodriguez katika muda wa mwisho wa usajili wa dirisha dogo. Nazo klabu za Crystal Palace na Hull City ni mojawapo ya vilabu vilivyopo katika harakati za kumfukuzia mshambuliaji Rickie Lambert mwenye umri wa miaka 32 kwa ajili ya kumsajili kwa mkopo. Winga wa klabu ya Dnipro Yevhen Konoplyanka mwenye umri wa miaka 25 amepiga chini ofa ya kujiunga na AS Roma ili aweze kuchukuliwa na aidha Liverpool au Spurs katika kipindi cha usajili wa kiangazi. Manchester United wanatarajia kuweka dau la kuondolea kama watafanikiwa kumshawishi golikipa David De Gea mwenye umri wa miaka 24 kusaini mkataba mpya. Wakati huohuo United wanaripotiwa kukaribia kumsajili beki wa Dynamo Kiev Aleksandar Dragovic mwenye umri wa miaka 23 pamoja na vilabu vya Italia kuonyesha kumuwinda pia. Kiungo wa klabu ya Borussia Dortmund Marco Reus anatarajiwa kutimkia Arsenal baada ya nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani kudai anataka kufanya kazi na meneja Arsene Wenger. Nazo Arsenal na Liverpool zimepewa ofa ya kumsajili beki wa Real Madrid Fabio Coentrao mwenye umri wa miaka 26 baada ya United kujitoa katika mbio za kumsajili lakini klabu hizo nazo zinaonyesha kutokuwa na nia ya kumchukua.

No comments:

Post a Comment