Sunday, February 1, 2015

STURRIDGE AMMWAGIA MISIFA STERLING.

MSHAMBULIAJI nyota wa Liverpool Daniel Sturridge ametoa ofa ya ulinzi kwa mshambuliaji mwenzake Raheem Sterling nje ya uwanja huku akidai anajivunia kiwango cha chipukizi huyo. Sturridge mwenye umri wa miaka 25 alifunga bao baada ya kurejea kutoka katika majeruhi jana katika ushindi wa mabao 2-0 waliopata dhidi ya West Ham United katika Uwanja wa Anfield baada ya Sterling kufunga bao la kuongoza. Sturridge ambaye alikuwa nje ya uwanja toka Septemba mwaka jana amesema Sterling amekuwa akifanya vyema na yote hiyo inatokana na juhudi zake anazofanya. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa akiwa kama kaka yake mkubwa anajivunia mafanikio aliyopata mpaka sasa na kuahidi kumsaidia wakati wowote atakapohitaji msaada wake. Baada ya kuanza msimu kwa kusuasua, Liverpool sasa imeimarika na kupata ushindi wake wa tano katika mechi sita zilizopita za Ligi Kuu hivyo kuweka hai matumaini yao ya kumaliza katika nafasi nne za juu.

No comments:

Post a Comment