Sunday, February 1, 2015

SARE YAMCHEFUA PELLEGRINI.

MENEJA wa klabu ya Manchester City, Manuel Pellegrini amesema amesikitishwa kwa kikosi chake kutoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Chelsea jana katika Uwanja wa Stamford Bridge. Pellegrini amedai kuwa kikosi chake kilistahili kupata matokeo zaidi ya hayo kwani ndio waliotengeneza nafasi nyingi zaidi ya waoinzani wao. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa kikosi chake kilikuwa kikijaribu kutafuta ushindi kuanzia mwanzo wa mchezo mpaka mwisho. Loic Remy ndiye aliyewafungia Chelsea bao la kuongoza kabla ya David Silva hajasawazisha muda mchache kabla ya mapumziko na kupelekea timu hizo kugawana alama katika mchezo huo.

No comments:

Post a Comment