Sunday, February 1, 2015

DROGBA ADAI KUENDELEA KUITUMIKIA CHELSEA NA MSIMU UJAO.

MSHAMBULIAJI nyota wa Chelsea, Didier Drogba amesema atabakia katika klabu hiyo msimu ujao pamoja na ukweli kuwa mkataba wake wa sasa unamalizika katika majira ya kiangazi. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 36 alirejea Stamford Bridge Julai mwaka jana baada ya kuzitumikia klabu za Shanghai Shenhua ya China na Galatasaray. Drogba ameshacheza mechi 27 nyingi akitokea venchi katika mashindano yote kwenye kikosi cha Jose Mourinho msimu huu na amedai kuwa bado anafurahia kuendelea kuitumikia Chelsea. Akihojiwa Drogba amesema mipango yake kwa mwaka ujao ni kuendelea kuitumikia Chelsea na sio vinginevyo. Katika mchezo wa jana dhidi ya Manchester City Drogba aliachwa benchi na kuingizwa dakika za mwishoni pamoja na kukosekana kwa Diego Costa anayetumikia adhabu yake.

No comments:

Post a Comment