Sunday, February 1, 2015

AFCON 2015: WENYEJI GUINEA YA IKWETA WAWATOA TUNISIA KIUTATAUTATA.

WENYEJI Guinea ya Ikweta jana walifanikiwa kuwatandika wakongwe Tunisia na kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika. Katika mchezo huo Tunisia ndio waliotangulia kupata bao lao la kwanza kupitia kwa Ahmed Akaichi lakini bao hilo lilirejeshwa katika dakika za mwishoni na kuufanya mchezo huo kumalizika kwa sare katika muda wa kawaida hivyo kwenda katika dakika za nyongeza. Mchezaji nyota wa mchezo huo Javier Balboa ambaye alifunga bao la kusawazisha kwa njia ya penati iliyoleta utata ndio aliyewainua tena mashabiki wa nyumbani kwa kufunga bao safi la mpira wa adhabu umbali mita 25 bao ambalo lilidumu mpaka muda wa mwisho wa dakika 30 za nyongeza. Sasa Guinea ya Ikweta wanatarajiwa kukwaana na na aidha Ghana au majirani zao Guinea katika hatua inayofuata. Mapema Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC waliwabamiza bila huruma majirani zao Congo Brazzaville kwa mabao 4-2 na kutinga hatua hiyo na sasa wanakabiliwa na aidha Ivory Coast au Algeria ambazo zinacheza baadae leo.

No comments:

Post a Comment