Friday, December 19, 2014

TANZANIA YAMALIZA MWAKA IKIWA NAFASI YA 105 KATIKA VIWANGO VYA FIFA.

TANZANIA inafunga mwaka ikikwea kwa nafasi saba mwezi huu katika viwango vya ubora duniani vinavyotolewa na Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA kila mwezi. Mwezi uliopita Tanzania ilikuwa imeshika nafasi ya 112 duniani huku kwa Afrika wakiwa nafasi ya 33, lakini mwezi huu mambo yamekuwa tofauti kwani wamekwea hadi nafasi ya 105 duniani huku kwa upande wa Afrika wakiwa nafasi ya 28. Viwango vingine kwa upande wa Afrika vinabaki vilivyokuwa mwezi uliopita ambapo Algeria bado wanaongoza kwa kuwa nafasi ya 18 wakifuatiwa na Tunisia katika nafasi ya 22, Ivory Coast wako nafasi ya tatu kwa kushika naafsi ya 28 duniani. Wengine ni Senegal waliopo nafasi ya 35 na tano bora kwa upande wa Afrika inafungwa na Ghana waliopo nafasi ya 37. Kwa upande wa tano bora duniani hakuna mabadiliko yeyote kwani Ujerumani bado wanaongoza waifuatiwa na Argentina katika nafasi ya pili, Colombia wako katika nafasi ya tatu huku ya nne ikishikiliwa na Ubelgiji, tano bora inafungwa na Uholanzi.

No comments:

Post a Comment