Saturday, December 20, 2014

STERLING ASHINDA TUZO YA GOLDEN BOY.

MSHAMBULIAJI nyota wa Liverpool, Raheem Sterling amefanikiwa kushinda tuzo ya Golden Boy kwa mwaka huu na kuwa Mwingereza wa kwanza kushinda tuzo hiyo toka Wayne Rooney aliposhinda mwaka 2004. Sterling ametwaa tuzo hiyo kwa umahiri wake uliomfanya kuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Liverpool huku akiwa amejihakikishia namba katika kikosi cha timu ya taifa. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 20, amewashinda chipukizi wenzake akiwemo Adnan Januzaj wa Manchester United na Hakan Calhanoglu wa Bayer Leverkusen pamoja an wachezaji wenzake wa Liverpool Lazar Markovic na Divock Origi. Akihojiwa Sterling aliuambia mtandao wa Liverpool kuwa ni mafanikio makubwa kushinda tuzo kama hiyo na ni jambo la furaha kwake na familia yake. Wachezaji wengine wlaiowahi kushinda tuzo hiyo ni pamoja na Lionel Messi, Cesc Fabregas na Sergio Aguero.

No comments:

Post a Comment