Tuesday, October 21, 2014

PISTORIUS JELA MIAKA MITANO KWA KUMUUA MPENZI WAKE.

MWANARIADHA nyota mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp bila kukusudia. Mbali na hukumu hiyo Jaji Thokozile Masipa aliyesoma hukumu hiyo pia amemzuia Pristorius kulimiki silaha kwa kipindi cha miaka mitatu baada ya kupatia na hatia ya kuitumia kinyume cha sheria. Kabla ya kutoa huku hiyo jijini Pretoria Jaji Masipa amesema suala hilo ni changamoto kubwa kwake kupata adhabu ambayo itaridhisha pande zote kwenye kesi hiyo. Upande wa mashtaka ulikuwa ukitaka mwanariadha huyo kupewa kifungo cha miaka 10 jela baada ya kupatika na makosa ya kuua bila kukusudia huku upande wa utetezi wakitaka apewe kifungo cha nyumbani cha miaka mitatu na pia apewe usaidizi na ushauri wa kubadili tabia. Pistorius alimuua mpenzi wake Steenkamp usiku wa kuamkia siku ya wapendao Februari mwaka jana kwa kumfyatulia risasi zaidi ya tatu bafuni na kudai kuwa alidhani alikuwa amevamiwa na majambazi nyumbani kwake.

No comments:

Post a Comment