Wednesday, September 17, 2014

SEEDORF KUIBURUZA AC MILAN MAHAKAMANI.

WAKILI wa Clarence Seedorf, Tiziano Treu amedai kuwa mteja wake yuko tayari kuipeleka klabu ya AC Milan mahakamani kuhusiana na mgogoro wa malipo. Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi aliteuliwa kuwa kocha wa Milan Januari mwaka huu baada ya Massimiliano Allegri kutimuliwa lakini alishindwa kuifanya timu hiyo ing’ae na kujikuta wakimaliza katika nafasi ya nane katika msimamo wa Serie A. Kutokana na matokeo hayo Milan iliamua kumtimua kiungo wake huyo wa zamani na nafasi yake kuchukuliwa na Filippo Inzaghi. Klabu hiyo imekuwa na kawaida ya kuwaondoa makocha wake kama wako likizo badala ya kusitisha mikataba yao hivyo ina maanisha kuwa Seedorf atahitajika kulipwa mpaka juni mwaka 2006 wakati mkataba wake utakapomalizika. Seedorf kwasasa yuko katika mazungumzo na klabu hiyo ilin kujaribu kutatua mgogoro huo lakini Treu anadhani suala hilo lazima litamalizika mahakamani. Treu amesema alikuwa akitegemea pande zote kumaliza tofauti zao kila mmoja kiwa ameridhika lakini kwa jinsi mkutano wa mwisho ulivyomaliza ni wazi suala hilo linaweza kumalizikia mahakamani. Milan kwasasa ndio wanaoongoza msimamo wa Serie A wakiwa wameshinda mechi zao mbili za awali chini ya Inzaghi.

No comments:

Post a Comment