Tuesday, August 19, 2014

RWANDA YAIKOMALIA CAF, YAAMUA KUKATA RUFANI KUPINGA KUONDOLEWA AFCON.

SHIRIKISHO la Soka nchini Rwanda-Ferwafa limethibitisha leo kuwa limekata rufani kupinga kuondolewa katika mechi za kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika mwakani kwa kosa la kumchezesha mchezaji anayetumia majina mawili tofauti. Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF lilitoa adhabu baada ya kukumfanyia uchunguzi mshambuliaji wan chi hiyo Dady Birori ambaye ananacheza katika klabu ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC akitumia jina la Agiti Tady Etekiama. Toka ilipotolewa adhabu hiyo Rwanda wamekuwa wakipinga adhabu hiyo wakidai kuwa mchezaji huyo alichukua uraia wan chi hiyo kwanza kabla ya huo wa DRC. CAF imedai katika uchunguzi wake imefanikiwa kugundua kuwa mshambuliaji huyo mzaliwa wa DRC alizaliwa Desemba 12 mwaka 1986 kama inavyoonyesha katika hati yake ya kusafiria ya Rwanda, wakati hati yake nyingine ya kusafiria ya Congo inaonyesha amezaliwa Desemba 13 mwaka 1990. Katibu mkuu wa Ferwafa Olivier Mulindahabi amesema mshambuliaji huyo alipata hati yake ya kusafiria ya Rwanda mwaka 2009 wakati ile ya DRC inaonekana ilitolewa mwaka 2013 jambo ambalo linamfanya kuwa mchezaji halali wa Rwanda. Mbali na adhabu hiyo ya kuindoa Rwanda CAF pia waliwapa nafasi Congo Brazzaville ambao walifungwa kwa matuta katika hatua ya tatu ya kufuzu, kuchukua nafasi yao katika kundi A ambalo linajumuisha nchi za Nigeria, Afrika Kusini na Sudan. Michuano ya Mataifa ya Afrika inatarajiwa kufanyika nchini Morocco kati ya Januari 18 hadi Februari 8 mwakani nchini Morocco.

No comments:

Post a Comment