Monday, August 18, 2014

NIGERIA YUFUZU MICHUANO YA AFRKA YA VIJANA KWA USHINDI WA MEZANI.

NIGERIA imefanikiwa kufuzu kushiriki michuano ya Vijana ya Afrika itakayofanyika nchini Senegal mwakani baada ya kupewa ushindi wa mezani kutoka na wapinzani wao Lesotho kushindwa kujitokeza katika mchezo uliopangwa kuchezwa Agosti 16 mwaka huu huko Kaduna. Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka barani Afrika-CAF Hicham El Amrani katika taarifa yake amedai kuwa uamuzi huo ulifikiwa jana kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo baada ya waamuzi waliotakiwa kuchezesha mchezo huo kutoa taarifa ya kutofika kwa Lesotho uwanjani kama ilivyopangwa. Mwamuzi alitumia kifungua cha 55 katika kanuni za mashindano hayo kinachoeleza kuwa kama timu haitafika uwanjani na kuvaa tayari kwa ajili ya mchezo kwa muda uliopangwa au kuzidisha zaidi ya dakika 15 anatakiwa kumaliza mchezo huo na kutoa taarifa yake ambayo itasubiria uamuzi wa mwisho kutoka kwa kamati ya maandalizi. Kwa matokeo hayo Nigeria wamepewa ushindi wa mezani huku mchezo wa marudiano ukifutwa kutokana na kukosekana sababu za msimu zilizoizuia Lesotho kucheza mechi hiyo. Awali kabla ya uamuzi huo kutoka Lesotho walituma barua kwa mashirikisho yote ikiwemo na CAF na lile la Nigeria kutoa taarifa za kutokwenda kwenye mchezo huo kutokana na hofu ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

No comments:

Post a Comment