Tuesday, August 19, 2014

ITALIA HAKUNA VIPAJI - CONTE.

KOCHA mpya wa timu ya taifa ya Italia, Antonio Conte amekiri nchi hiyo haina vipaji kama mataifa mengine na kuwapa changamoto ya kufanya kazi kwa pamoja ili waweze kupunguza pengo dhidi ya timu bora. Kocha huyo wa zamani wa Juventus alitangazwa kuchukua nafasi ya Cecare Prandelli wiki iliyopita ambaye alijiuzulu baada ya Italia kutolewa katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil. Conte amesema amefirahi kupata kibarua hicho na anampongeza Prandelli kwa kazi nzuri katika kipindi cha miaka minne alichoifundisha nchi hiyo huku akimtakia kila la kheri katika klabu yake mpya ya Galatasaray. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa anapenda kushinda lakini amekiri kuwa nchi zingine zina wachezaji wenye vipaji zaidi yao hivyo jambo pekee wanaloweza kupunguza pengo hilo ni kucheza kitimu.

No comments:

Post a Comment