Tuesday, August 19, 2014

BAYERN MWAKA WA TABU, SCHWENSTEIGER NAYE PANCHA.

MWENYEKITI wa klabu ya Bayern Munich, Karl-Heinz Rummenigge amedai kuwa kiungo mahiri wa timu hiyo Bastian Schweinsteiger atakuwa nje kwa wiki mbili kutokana na kusumbuliwa na majeruhi ya goti. Kiungo huyo ambaye amekuwa akisumbuliwa na majeruhi katika goti lake la kushoto kwa miezi kadhaa hatua iliyopelekea kuhitaji matibabu katika michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika Brazil, bado hajafanikiwa kucheza mechi yoyote msimu huu. Rummenigge amesema madaktari wa timu hiyo wana uhakika tatizo la mchezaji huyo haliweza kuwa la muda mrefu hivyo katika kipindi cha wiki moja au mbili anaweza kuwa fiti. Kuna uwezekano mkubwa Schwensteiger ahaukosa mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya Ujerumani dhidi ya Argentina utakaochezwa Septemba 3 mwaka huu sambamba na mchezo wa kufuzu michuano ya Ulaya 2016 dhidi ya Scotland siku chache baadae.

No comments:

Post a Comment