Thursday, April 17, 2014

TEVEZ AKANUSHA KUWA NA UGOMVI NA MESSI.

MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Juventus, Carlos Tevez amesisitiza kuwa hana tatizo lolote na nyota wa Barcelona Lionel Messi kuhusu tetesi kuwa wamezozana na nahodha huyo wa Argentina. Kumekuwa na taarifa kuwa Tevez amepoteza nafasi yake katika kikosi cha timu ya taifa ya Argentina kwasababu na uhusiano mbovu alionao na Messi lakini Tevez mwenyewe amepuuza tetesi hizo. Akihojiwa Tevez amesema hajui hizo tetesi za kuwa na mahusiano mabaya na Messi zimetoka wapi lakini ukweli ni kwamba hana tatizo lolote na nyota huyo. Tevez amesema wamefanya mambo mengi pamoja ikiwemo kufanya mazoezi pamoja, kucheza pamoja na kumekuwa hakuna tatizo lolote kwasababu Messi ni mtu mzuri huku akimtakiwa kila la kher katika michuano ya Kombe la Dunia baadae mwaka huu. Nyota huyo ambaye pia amewahi kucheza katika timu ya Manchester City, ameichezea Argentina mechi 64 lakini hajajumuishwa katika kikosi cha nchi hiyo toka mwaka 2011.

No comments:

Post a Comment