Thursday, April 17, 2014

FEDERER HATI HATI KUSHIRIKI FRENCH OPEN.

MCHEZAJI tenisi bingwa mara 17 wa michuano ya Grand Slam, Roger Federer amedokeza kuwa anaweza asishiriki michuano ya wazi ya Ufaransa ili aweze kuwa na mke wake wakati atakapojifungua kwa mara nyingine. Federer mwenye umri wa miaka 32 ana watoto mapacha na mkewe Mirka na Desemba mwaka jana alisema kuwa wanetegemea mtoto wa tatu ingawa hakusema lini. Akihojiwa Federer amesema ni jambo la muhimu kwake kuwepo pale na kumsaidia mke wake kwa kila hali. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa amecheza mechi za tenisi za kutosha hivyo kukosa michuano fulani haitabadilisha chochote kwake. Akiulizwa kama kauli hiyo inamaanisha kuwa anajiandaa kuikosa michuano hiyo ya Ufaransa ambayo inatarajiwa kuchezwa kuanzia Mei 25 hadi Juni 8, Federer ambaye ni raia wa Uswis alidokeza kuwa inawezekana kama wakati utakuwa umefika.

No comments:

Post a Comment