Thursday, April 17, 2014

DRAXLER HAONDOKI SCHALKE - WAKALA.

WAKALA wa mshambuliaji wa Schalke, Julian Draxler amesema kuwa mteja wake huyo anaweza kubakia katika timu hiyo kwa msimu mwingine zaidi. Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger alikuwa akimfukuzia nyota huyo mwenye miaka 20 katika dirisha dogo la usajili Januari mwaka huu na kukaribia kufikia makubaliano kabla ya uhamisho huo kushindikana dakika za mwisho kabla ya dirisha halijafungwa. Arsenal walitegemewa kuanza upya kumfuatilia kinda huyo wa kimataifa wa Ujerumani katika majira ya kiangazi lakini wakala wake Roger Wittman anategemea kuwa mteja wake atabakia kwenye timu hiyo kwa msimu mwingine pamoja na kutakiwa na vilabu vingi vikubwa. Wittman amesema anadhani itakuwa vyema kwa chipukizi huyo kubakia katika klabu hiyo iliyomkuza ili aweze kukomaa zaidi kabla ya kuamua kutoka na kwenda sehemu nyingine.

No comments:

Post a Comment