Thursday, April 17, 2014

BAYERN BADO INAHITAJI KUNOA MAKALI YAKE - SAMMER.

MKURUGENZI wa michezo wa klabu ya Bayern Munich, Matthias Sammer amesisitiza kuwa timu hiyo inatakiwa kukuza mchezo wake kama wanataka kunyakuwa mataji matatu msimu huu huku akidai wachezaji wamekuwa wa pole sana. Bayern jana waliichabanga Kaiserslautern kwa mabao 5-1 na kujikatia tiketi ya kucheza fainali ya DFB Pokal dhidi ya Borussia Dortmund lakini Sammer anaonyesha hakufurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na timu hiyo. Summer amesema wamefurahishwa na timu hiyo kutinga fainali lakini hakufurahishwa na jinsi walivyocheza. Nguli huyo wa zamani wa soka wa Ujerumani amesema kumekuwa na makosa mengi ya kizembe katika mchezo huo na hiyo inasababishwa na wachezaji wenyewe kushindwa kukumbushana majukumu yao pindi wawapo uwanjani. Sammer amesema kama wachezaji wakiweza kukumbushana majukumu yao hakuna shaka kwamba kiwango lazima kitapanda.

No comments:

Post a Comment