Friday, September 1, 2017

CHELSEA YAWANASA DRINKERWATER NA ZAPPACOSTA DAKIKA ZA MAJERUHI

MABINGWA wa Ligi Kuu Uingereza, Chelsea imekamilisha usajili uliokuwa na changamoto nyingi Alfajiri ya leo kwa kuwanasa kiungo Danny Drinkwater kutoka Leicester City na beki wa kulia wa kimataifa wa Italia Davide Zappacosta kutoka Torino. Meneja wa Chelsea Antonio Conte alishuhudia mawindo yake kadhaa yakishindikana katika muda wa mwishoni wa usajili wa kipindi hiki cha kiangazi lakini alifanikiwa kuimarisha kikosi chake kuelekea michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Drinkwater mwenye umri wa miaka 27 amesajiliwa kwa mkataba wa miaka mitano na ada inayokadiriwa kufikia paundi milioni 35, ambayo ilitangazwa saa mbili na nusu baada ya dirisha la usajili kufungwa jana usiku. Zappacosta mwenye umri wa miaka 25 amesajiliwa kwa mkataba wa miaka minne na Chelsea wametoa paundi milioni 23 kunasa saini ya beki huyo. Mbali na hao Chelsea pia ilifanikiwa kuwasajili mapema kipa Willy Caballero, beki Antonio Rudiger, kiungo Tiemoue Bakayoko na mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania Alvaro Morata aliyejiunga nao kutoka Real Madrid kwa ada iliyovunja rekodi ya klabu ya paundi milioni 58.

COUTINHO AITAKATISHA BRAZIL

TIMU ya taifa ya Brazil, imefanikiwa kujihakikishia nafasi ya kumaliza kinara katika mechi za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia huko Amerika Kusini baada ya kuichapa Ecuador jana wakati Chile na Argentina zikiendelea kusuasua kwa mara nyingine. Brazil ilishinda mchezo huo kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na nyota wa Liverpool Philippe Coutinho ambaye usajili wake kwenda Barcelona ulikwama pamoja na Paulinho ambaye amesajili kipindi hiki cha kiangazi na Barcelona akitokea Shanghai Evergrande ya China. Ushindi huo unakuwa wa tisa mfululizo kwa Brazil na kuwapata mabingwa mara tano wa Kombe la Dunia uhakika wa kumaliza kinara kutokana na tofauti ya alama 11 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine. Timu nne kutoka ukanda huo ndio zinafuzu moja kwa moja michuano hiyo ijayo inayofanyika nchini Urusi mwakani huku ile ya tano ikienda kucheza hatua ya mtoano. Katika michezo mingine iliyochezwa mapema leo Alfajiri, Colombia walitoka sare tasa na Venezuela, Peru waliididimiza Bolivia mabao 2-1, Paraguay ikaishughulikia Chile kwa kuitandika mabao 3-0 na Argentina walitoka sare ya bila kufungana na Uruguay.

PALACE YAMCHUKUA SAKHO MOJA KWA MOJA

KLABU ya Crystal Palace imefanikiwa kumsajili beki wa kati Mamadou Sakho kutoka Liverpool kwa kitita cha paundi milioni 26. Ofa hiyo ilikuwa ya nne kwa Palace kwa ajili ya kumuwania beki huyo mwenye umri wa miaka 27 baada ya Jumanne kukataliwa ofa yao ya paundi milioni 25. Liverpool walieleza kuwa hawatakubali kuchukua ofa chini ya paundi milioni 30 kwa ajili ya nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa ambaye alicheza kwa mkopo Selhurst Park msimu uliopita. Akizungumza na wanahabari mara baada ya kumalika kwa usajili huo, Sakho amesema anapenda changamoto aliyopata msimu uliopita, ilikuwa vigumu lakini ilimvutia ndio maana akaona sehemu sahihi ya kwenda ni Palace kipindi hiki cha kiangazi.

PSG YAMCHUKUA MBAPPE KWA MKOPO

KLABU ya Paris Saint-Germain-PSG imefanikiwa kumsajili Kylian Mbappe kwa mkopo wa msimu mzima kutoka Monaco huku kukiwa na kipengele cha kumnunua kwa mkataba wa moja kwa moja kwa euro milioni 180. Kama PSG wakimsajili nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa kwa mkataba wa moja kwa moja, mkataba utakuwa unamalizika Juni mwaka 2022. Akizungumza na wanahabari, Mbappe amesema alikuwa akitaka kuwa sehemu ya mpango wa klabu hiyo ambayo ni moja ya klabu zenye kutaka mafanikio makubwa Ulaya. Kuchelewa kwa Mbappe kusaini mkataba wa kudumu kunadaiwa kumetokana na PSG kuogopa kuvunja sheria ya matumizi ya fedha ya Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA ambayo inavitaka vilabu vyote kutotumia zaidi ya fedha inayoingiza.

KUIONA STARS BUKU TANO

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetangaza viingilio vya mchezo kati ya Taifa Stars ya Tanzania na Botswana utakaofanyika Jumamosi Septemba 2, mwaka huu. 

Mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam chini ya utaratibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) viingilio vitakuwa Sh 10,000 kwa Jukwaa Kuu na Sh 5,000 kwa mzunguko.

Wakati huo huo, Kiungo Taifa Stars, Simon Msuva tayari amejiunga na timu hiyo akitokea Klabu ya Difaa El Jadidah ya Morocco baada ya Shirikisho la Soka Morocco na timu yake kumfanyia mpango wa visa ya muda mrefu iliyomwezesha kusafiri.

Mchezaji ambaye imeshindikana kuja ni Orgenes Mollel wa FC Famalicao ya Ureno. Sababu ni taratibu za ruhusa za kimataifa zinafanyiwa kazi kwa mujibu wa sheria za nchi ya Ureno ambako anacheza soka la kulipwa.

Nyota wengine walikwisha kuripoti ni pamoja na Nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji), Elias Maguli (Dhofar FC/Oman), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya) wakati Farid Mussa wa CD Tenerif ya Hispania anatarajiwa kutua leo.

Wengine ambao wako kambini Hoteli ya Sea Scape iliyoko Kunduchi, Dar es Salaam ni makipa Aishi Manula (Simba SC), Mwadini Ally (Azam FC) na Ramadhani Kabwili (Young Africans).

Pia wamo Walinzi ni Gadiel Michael (Young Africans), Boniphas Maganga (Mbao FC), Kelvin Yondani (Young Africans), Salim Mbonde (Simba SC) na Erasto Nyoni (Simba SC).

Viungo ni Himid Mao – Nahodha Msaidizi (Azam FC), Mzamiru Yassin (Simba SC), Said Ndemla (Simba SC), Shiza Kichuya (Simba SC), wakati Washambuliaji ni Raphael Daud (Young Africans), Kelvin Sabato (Azam FC) na Emmanuel Martin (Young Africans).

Katika hatua nyingine, Botswana inatarajiwa kuingia usiku wa saa 3.00 kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ) na watafikia Hoteli ya Urban Rose iliyoko katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Botswana inayonolewa na David Bright inakuja na wachezaji 18 wakiwamo makipa Mampule masule, Noah Maposa na Antony Gouws.

Walinzi ni Letsweletse, Mosha Gaolaolwe, Simisane Mathumo, Thabang Mosigi, Lesenya Ramorake, Tapiwa Gadibolae na Bokani Leeton.

Viungo ni Alphonse Modisaotsile, Maano Ditshupo, Katlego Masole, Gift Moyo, Segolame Boy, Lemponye Tshireletso, Thero Setsile, Kabelo Seakanyeng,Jackson, Lemogang maswena.

Washambuliaji ni Tumisang Orebonye, Jarome Ramathakwane, Tebogo Sembowa, Hendric Moyo na Boipelo Oaitse.

Friday, August 25, 2017

RATIBA YA MAKUNDI YA EUROPA LEAGUE

Kundi A: Villarreal, Maccabi Tel Aviv, Astana, Slavia Prague.
Kundi B: Dynamo Kiev, Young Boys, Partizan Belgrade, Skenderbeu.
Kundi C: Sporting Braga, Ludogorets, Hoffenheim, Istanbul Basaksehir.
Kundi D: AC Milan, Austria Vienna , Rijeka, AEK Athens.
Kundi E: Lyon, Everton, Atalanta, Apollon Limassol.
kundi F: FC Copenhagen, Lokomotiv Moscow, Sheriff Tiraspol, FC Zlin.
Kundi G: Vitoria Plzen, Steaua Bucarest, Hapoel Beer-Sheva, FC Lugano.
Kundi H:Arsenal, BATE Borisov, Cologne, Red Star Belgrade.
Kundi I: Salzburg, Marseille, Vitoria Guimaraes, Konyaspor.
Kundi J: Athletic Bilbao, Hertha Berlin, Zorya Luhansk, Ostersund.
Kundi K: Lazio, Nice, Zulte Waregem, Vitesse Arnhem.
Kundi L: Zenit St Petersburg, Real Sociedad, Rosenborg, Vardar.

RATIBA YA MAKUNDI YA CHAMPIONS LEAGUE

Kundi A: Benfica, Manchester United, Basel, CSKA Moscow
Kundi B: Bayern Munich, Paris St-Germain, Anderlecht, Celtic
Kundi C: Chelsea, Atletico Madrid, Roma, Qarabag
Kundi D: Juventus, Barcelona, Olympiakos, Sporting
Kundi E: Spartak Moscow, Sevilla, Liverpool, Maribor
Kundi F: Shakhtar Donetsk, Manchester City, Napoli, Feyenoord
Kundi G: Monaco, Porto, Besiktas, RB Leipzig
Kundi H: Real Madrid, Borussia Dortmund, Tottenham, Apoel